Ijumaa 20 Februari 2026 - 11:00
Muqawama wa Kiislamu bado ni wenye nguvu na madhubuti

Hawza/ Mjumbe wa kambi ya Baalbek-Hermel amesisitiza kuwa Mapambano ya Kiislamu, licha ya shinikizo kubwa la kifedha, kiuchumi na kisiasa lizoelekezwa dhidi yake, bado ni yenye nguvu na madhubuti.

Kwa mujibu wa taarifa ya Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Ibrahim al-Mousawi, mbunge na mjumbe wa kambi ya Baalbek-Hermel, katika hotuba yake aliyotoa wakati wa mkutano wa kisiasa ulioandaliwa na Idara ya Uhusiano wa Umma ya Hezbollah katika mji wa Hourtala, alisisitiza kuwa; Mapambano ya Kiislamu, pamoja na kuwepo kwa mashinikizo makubwa ya kifedha, kiuchumi na kisiasa dhidi yake, bado ni yenye nguvu na thabiti. Aliongeza kuwa; kama utawala wa Kizayuni ungekuwa na uwezo wa kutuangamiza, bila shaka ungalifanya hivyo; lakini kwa fadhila za Mwenyezi Mungu, kamwe hautaweza kufanya hivyo.

Alihoji: Ikiwa mnasema sisi tumeshindwa, basi kwa nini kupitia wapatanishi mnatafuta kufanya mazungumzo nasi kuhusu silaha za muqawama? Marekani na wafuasi wake wote ni wanafiki na wenye kujifanya.

Al-Mousawi aliendelea kubainisha kwamba; uimara na msimamo thabiti wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran pamoja na msimamo wa Kiongozi Mkuu, Ali Khamenei, ambaye hajawahi kulegeza wala kuonesha udhaifu hata mara moja, ndicho kilichochelewesha uchokozi dhidi ya Iran. Iran ni taifa lenye nguvu, thabiti na lenye uwezo mkubwa, na liko tayari kujibu aina yoyote ya uchokozi.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha